Pages

Mwogozo Wa Damu Nyeusi Part 3



GILASI YA MWISHO MAKABURINI

  Katika hadithi hii tunapatana na Msoi  mwenye utambuzi wa kipekee ya mamabo yatakayotokea. Msoi alipata hisia flani yenye kitisho na wasiwasi. Ndoto nyingi ambazo Msoi aliwahi kuota mara mara hua ingawa marafiki wake hawakuamini.
  Hisia hizo ambazo Msoi alijaribu kuepuka kwa muda kwa mwezi mmoja hatimaye zilimfanya awe mwoga zaidi yeye pamoja  na marafi zake walikuwa wanaenda katika bar iliyokuwa kwenye maskani ya mava ili kunywa  na kujiburudisha  baada ya kazi. Pia pahali hapo palipopachikwa jina la kimombo exotic resort.
  Siku moja aliamua kutoenda katika mava kwani hisia zake zilimfanya aogope sana. Kwa sababu aliona kwamba balaa kubwa itatokea,Semkwa rafikiye Msoi alienda kwake nyumbani ili kumsihi waende katika mava akaitikia shingo upande. Walipokuwa wakitokea Msoi aliligonga bakuli la maua likavunjika vipande vipande ,alikuwa karibu kuanguka akiteremsha mguu na pia alijibana kidole  kidogo kwenye mlango wa gari. Hizi zilikuwa ishara za kuonyesha kwamba jambo mbaya litatendeka.
  Njiani walisikia mgurumo wa radi ambayo Semkwa aliona kuwa jambo la kawaida. Walipofika kwenye daa ya makaburini,walipatana na Asha na Josefina. Walipokaa  chini,Msoi aligeuza namna yake ya kukaa. Siku hiyo alitaka  kuyaangalia mava ili jambo likitokea ataweza kutoroka.
  Muda ulivyozidi kuyoyoma , Msoi na marafiki wake walijiburudisha na vinywaji  na muziki  uliochezwa na bendi. Asha na Msoi walipokuwa wakichheza densi, Msoi alionekana mwenye wasiwasi. Wenzake wakaanza kumtani hadi ikambidi anyamaze ili angoje kile ambacho kitaendeea. Msoi alingwa na kuburudika nao ijapokuwa walimtani na kumkejeli  kuhusu ndoto zake. Asha aliburudishwa na Msoi kuhusu  matukio yaliyotendeka na Msoi kuhusu matukio yaliyotendeka awali ambayo aliona kama ni ya bure tu. Msoi aliamua kujinyamazia.
Wakati ambao kila mtu alikuwa ameshiba walicheza mziki huku wakiwa kwani hawakutosheka. Baada ya muda mfupi, Msoi aliviona vizuu vimejifufua kwa mtindo wa Thriller  wa Micheal Jackson, Asha alipiga uyoe ambao uliskika na kila mtu. Watu walipoona yaliyokuwa yakiendelea walitimua mbio hadi kwao nyumbani. Wengine walianguka na kukanyang’wa
Baada ya Asha na Msoi kufika nyumbani waliskia habari kwenye televisheni kwamba wale vizuu walikuwa majambazi ili waibie Baa ya Makaburini pamoja na wateja wao.kwa mara nyingine marafiki zake Msoi walifahamishwa kwamba wanafaa  kumsikiliza.
DHAMIRA.
Ø Mwandishi  anatuhimiza tusipuuze mambo ambayo  tunaonywa na marafiki zetu.
MAUDHUI
Ø  ANASA NA STAREHE
Tunaona  kwamba Msoi na Asha walikuwa wanaenda kwenye baa ya makaburini kujiburudisha baada ya kazi na kulewa kiasi cha kujisahau.
Ø  UHALIFU
Majambazi walivamia watu na  kuwaibia mali yao kwani waligundua kwamba watu huogopa wafu
Ø  ITIKADI NA USHIRIKINA
Ushirikina ni ile hali ya kuamini nguvu nyingine kuliko mungu
Msoi aliamini kwamba baa iliyokuwa kwenye mandhari ya mava ingevamiwa na watu wasiojulikana
Ø  URAFIKI NA UTANGAMANO
Akina Semkwa,Msoi,Asha na Josephina waliburudika pamoja na kutengamana.walifanya m ambo pamoja
Ø  UWOGA
Msoi aliota ndoto ambazo zilimfanya awe mwoga.
WAHUSIKA
1.Msoi.
Ni mtu mwenye kipawa utambuzi wa mambo
SIFA
       I.            Ni mbarazi ,ana mazoea ya kukaa na watu wengine hasa katika baa.
     II.            Ni mshiriki anasa,amekuwa akizuru bar ya makaburini ili kustarehe.
  III.            Ni mpole,hana mambo mengi.
  IV.            Ni mwoga.
    V.            Ni mshirikina,anaamini katika mambo ya ushirikina.
  VI.            Anashawishika kwa urahisi.
2.Semkwa,Asha na Josefina.
       I.            Ni wabaraza
     II.             Wapenda anasa,kila wikendi walikuwa wanakutana katika baa na kuburudika pamoja.
  III.            Wabishi,walibishana na Msoi alipowadokezea kuhusu ndoto yao.
  IV.            Weye utani ,wanamtania Msoi anapowaeleza kuhusu ndoto yake.


3.Majambazi.
         I.            Ni watu wabunifu –walivaa kama wafu ili waweze kuwaogofya watu
      II.            Ni waoga-hawajitokezi moja kwa moja kukabiliana na watu.
    III.            Wahalifu –walijaribu mali ya watu baada ya kuwaibia.

KIKAZA.

Hadithi hii inazungumzia kikaza ambacho ni suruali spesheli. Kikaza hiki kimetumiwa kusimamia uongozi katika jamii. Kikaza ni jazanda inayosimamia  uongozi. Hadithi inaanza pale ambapo kuna dalili za mvua kunyesha,lakini Mzee Babu akawafahamisha wanakijiji kwamba haitanyesha. Kwanza wanatekede hawakuamini. Kulikuwa na kikao kwa mzee huyu na miongoni mwa waliohudhuria ni Bi Cherenga almaarufu Bi Cherehani na Bw Pima,Bw Machupa pia alikuwepo(msemaji wa kijiji). Wote walitaka Mzee Babu awafunulie kitendawili.
Washona kikaza ni wananchi wenyewe. Kikaza kilikuwa kimepasuka. Bw Mtajika(kiongozi) alifanya makosa kumwacha  Bi Mtajika kukiguza kikaza,kwani yeye siye kiongozi. Mapinduzi ni marekebisho yalihitaji kufanywa. Kulikuwa nia uongozi mbays. Bw Pima alipima kikaza na Bi Cherehani kukishona. Bi Cherehani  aliwahimiza  wanatekede  kwenda  kukishona kikaza  (kurekebisha makosa na kumtoa  Bw Mtajika  mamlakani) . Kikaza kilihitaji kushonwa. Bi Cherehani  alihakikisha kwamba atapunguza kipimo ili kikaza kikaze. Kikaza (uongozi) ni cha ushirika.
DHAMIRA.
Mwandishi anataka kuonyesha kwamba uongozi ni  ushirika.
MAUDHUI
1.UONGOZI
Hadithi  hii inaongea kuhusu  swala la uongozi.

·        Uongozi  umewakilishawa na kikaza – “suruali  ya ndani”
·        Uongozi hushonwa na wananchi.
·        Uongozi ni ushirika.
·        Uongozi mzuri au mbaya hutokana na mchango wa watu wenyewe
·        Mwandishi pia anaguzia swala la uongozi mbaya
·        Bw Mtajika tunaelezwa kwamba kikaza chake kimeraruka na basi uongozi umeigiza dosari.
·        Bi Mtajika amechangia katika uongoza mbaya.
·         Wanawake walishona kikaza  kiliochobana
2.UBINAFSI
Bw Mtajika na wenzake waliochaguliwa waliochaguliwa waliwasahau  waliwasahau wenzao waliowachagua kama vile kobe alivyowatendea hadithi yake kuenda angani.


3.USHIRIKIANO
Kikaza kilishonwa kwa kushirikiana. Katika uongozi, lazima pawepo na ushirikiano wa watu wote.

4. MABADILIKO

Baada ya mambo kugonga mwamba, viongozi wanatolewa mamlakani na kubadili uongozi.

5. USALITI

Bwana mtajika na Bi. Mtajika , anawasaliti wananchi kwa kuongoza vibaya na kutomzuia mkewe kukigusa kikaza.

6. UKARIMU

Babu na wanakijiji ni wakarimu wanapopeana mavuno.

7. KUTOWAJIBIKA

Viongozi hawakuajibika katika uongozi wao.

8. UTABIRI

Babu anatabiri.

WAHUSIKA

1.   MZEE BABU

·        Ni mtabiri
·        Mkarimu
·        Mwenye busara . Anawatetea na kuwashauri watu
·        Mbaraza. Anapenda kuingiana na watu.
·        Mtambuzi wa mambo.

2.                       BW. MTAJIKA

Kiongoziwa tekede.

SIFA

1.     Ni mweledi wa kuongea .anapoongea, hawei kubadilisha ukweli kuwa uongo.
2.     Mwenye ubinafsi. Alipopata cheo, aliwasahau wengine.
3.     Ni mwanamme anayetawaliwa na mkewe. Alikua amezidiwa na nguvu za pili.
4.     Msailiti. Amewasaliti wananchi wa Tekede kwa kuwasahau (hadithi ya safar ya mzee kobe kwenda angani. )

3.      BI CHEREHANI/ BI CHIRENGA.

·        Mshonaji kikazi.
·        Ni mnyamavu kwani hapendi kuzungumza
·        Ni mwenye soni
·        Mkweli. Hapiti njia mbili. Hafichi mambo.
·        Ni mzalendo .hakwenda ikuliuni peke yake.
·        Mwenye bidii kwani anashona kikaza kama jukumu lake.
·        Mvumilivu. Amevumilia kukemewa na watu.

4.      BI MTAJIKA.

Msaliti anakigusa kikaza ingawa anaelewa itikada ya jamii ya wana Tekede inayosema kwamba wa pili hafai kugusa kikaza.
Ni mkoloni kwani anaamua kutawala watu apendavyo yeye.


5.     WANAKIJIJI

Ni wakarimu.Walimpa babu mavuno waliyoyapata.
Wenye mapinduzi. Watu walizinduka kuhusu uongozina Bw. Mtajika.
Ni wenye ushirikiano.Wanashirikiana kumtoa Bi Mtajika kwenye mamlaka.
Ni wasikivu. Wanamsikiliza babu kwa makini.
Ni wenye utamaduni.Wanatii tamaduni zao.K.m bibi hakustahili kugusa kikaza.

 

MBINU ZA LUGHA


a)      TASHTITI
Ni mbinu ya kukejeli mtu kwa njia ya kutomuudhi moja kwa moja.
Hadithi ya kobe ni tashtiti murua inayoonyesha ubadhilifu, ukaidi na uogozi mbaya wa Bw. Mtajika. Mzee Babu anawapa watu hadithi badala ya kusema yote aliyoyafanya kombo Bw. Mtajikana adhabu atakayoipata atakaposhushwa madaraka.
Ushonaji wa kikaza vibaya kwa Bi. Cherehani na Bw. Pima pia ni tashtiti. Yaonyesha namna ambavyo wanakijiji wa Tedeke waliomchagua kiongozi aliyefaa.
Msemo wa nyani haoni kundule ni semi linaloeleza upambano na kutojali kwa wanakijijij wa Tekede.
b. FUMBO
Kikaza kimetumika kimafumbo kumaanisha uongozi, upimaji Na kushonwa kwa kikaza ni kumteua na kumtwika majukumu ya uongozi. Kupima na kushona kikaza ina maana ya ushirikiano wa jamii katika kumchagua na kumsimika kiongozi.
Wa pili hakuruhusiwa kushika kikaza ni mke wa kiongozi. Kutanda Kwa mawingu meusi angani kusha kukosa kunyesha ni fumbo inayoeleza dhiki ya waakaazi wa Tekede.

c. HADITHI
Hadithi katika hadithi hii inamhusu kobe inayosimuliwa na mzee Mzee Babu. Musiliko wa karamu angani ilimjulisha kobe, ndege na kadhalika. Mzee kobe alifanya ujangili na kudai jina sisi sote.
Kila chakula, kinywaji na starehe zilielekezwa kwake. Ndege walitababika na kuamua kumnyanyanya kobe. Manyoya yao na kobe hakuweza kupaa tena ndio maana gamba la kobelena viraka au mipasuko.
D. MAJAZI
Mbinu za kisanaa.
Baadhi ya wahusika wanapewa majina kulingana na sifa au hulka zao. K.m. Mzee Babu alikuwa mzee kuliko wengine. Bw. Mtajika alitojwa mara kwa mara na kila mtu kwa sababu alikua kiongozi wao. Bw.Machupa pima aliyapima kwa uangalifu alivyowaambiwa wanakijiji.
Bw Machupa hakuwa na msimamo dhabiti hasa kuhusu uongozi wa Bw. Mtajika.
e. TAKRIRI
Baadhi ya kauli zimekaririwa ili kutilia mawazo Fulani mkazo k.m Bw. Cherehani na Bw. Pima walikuwepo kushiriki na kutoa  mchango walikuwepo vilevile.
Kitendawili cha kukaza kikazidi kukazaa.

f. TABAINI

Ni kusisitiza mambo kwa kutumia vikarushi. Baadhi ya semi zina dhana ya ukinzani lakini kwa hakika hakuna ukinzani kimaana. K.m si salama si chochote hakuna kilichotaka kinywani.

g. TASHBIHI

Yaliyopita huja kama nguvu za sunami.(uk 45) Machupa hutafuna na kupuliza kama panya.

h. BALAGHA

Hayahitaji majibu.
Anasema nini?
Itakuwaje sisi wawili ndio tuwe najibu?

6.     MAEKO

Hadithi inapoanza ni usiku wa manene ambapo Hamduni au Duni anaporejea kwake. Anatoka ulevini kama ilivyokuwa desturi yake. Ni majira ya usiku wa manane.  Anaimba wimbo wake wa kawaida ambao mwandishi anaita “taarabu njia.” Kwani alizoea kuuimba akiwa njiani kuelekea kwake.
Jamila mkewe Hamduni anapomsikia mumewe anamka ili kumsubiri. Mwanzoni mumewe anamka ili kumsubiri. Mwanzoni mumewe anaonyesha furaha na bashasha kwa kupokelewa na mkewe. Lakini anageuka na kuwa mjeuri mkewe anapojaribu kumsaidia kupanda ngazi za kuingia kwao puia anampiga mkewe teke kwa kukawia kumpatia chakula.
Mwandishi anasema ghasia na zogolaukorofi wa duni zilidi na kukosesha utulivu katika ndoa yao. Majirani na hata jamaa zake jamila walipoona kipigo kimezidi walimshauri ajiondoe kwenye ndoa hiyo. Hata kuna kifana kwa jina salim aliyoyapitia. Alitaka Jamila amwasi duni halafu angetoroka naye.Alishindwa kuelewa Kwa hakika. Salim alimpenda kwa dhati au alitaka kujinufaisha kutokana na hali yake Jamila.
Kwa sababu ya madhila aliyofanyiwa  na mumewe Jamila ya kawaida. Alirauka asubuhi na kutayarisha kiamsha kinywa cha kukata na shoka ambacho alikiagizwa kwa fujo. Kenyoye Duni alimpumbaza mkewe kwa mapenzi yasiyo ya kawaida. Alirauki asubuhi na kutayarisha  kiamsha kinywa cha kukata na shoka akakusanya nguo zote chafu na kuziroweka ili azifue baadaye kasha akaenda kumwita mkewe. Alimuomba msamaha mkewe kwa yale yote aliyomtendea kasha wakashebeha.
Baada ya hapa maisha yakawa ni yay ohayo amani na mapenzi kwa muiezi miwili, kufarakana, kuombana msamaha, amani na kadhalika.Hta Jamila mwenyewe alishindwa afanye nini. Lakini kwa kiasi kikubwa aliridhishwa na ndoa yake licha ya matatizo aliyoyapata humo.

DHAMIRA

Watu huvimilia mapato wanayoyapata katika ndio hiyo k.m. jina, pesa, mapenzi na kadhalika.

MAUDHUI

1.     ULEVI

Unywaji pombe kupindukia.
Hamduni alilewa kupita kiasi.Mwandishi anataka kukashifu ulevi.

2.     UVUMILIVU

Jamila amevumilia mateso na majirani wanavumilia kero za hamduni.

3.     DHULMA KATIKA NDOA

Hamdunio anamwacha mkewe na kwenda kulevya.
Kumchapa Jamila akiwa amelevya.

4.     MAEKO

Namna ambavyo mtu (Jamila) amewekwa.
Jamila anavumilia dhulma za ndoa kwa kuwa anapewa pesa, mapenzi, anafanyiwa kazi.

WAHUSIKA


1.HAMDUNI

Ni mhusika mkuu katika hadithi hii na ni mumewe Jamila.

SIFA

1.     MLEVI

Analewa kila siku

2.     Mwenye fujo

Anampiga mkewe.

3.     Ni mkaidi

Alikanywa kupiga makelele usiku lakini anazidisha.

4.     Ni msumbufu

Aliimba usiku watu wakiwa wamelala.

5.     Ni msanii

Alipenda kuimba.

6.     Ni mwenye majuto

Hujitia makosa ambayo alitenda akiwa amelala.

7.     Ni msahaulifu

Anasahau kwa haraka aliyomfanyia mkewe.

8.     Ni mwenye mapenzi.

Anampenda mkewe.

 

 

 

2. JAMILA

Mhusika mkuu ni mkewe Hamduni.

SIFA

1.     Mwanamke mwenye umri mdogo.
2.     Ni mvumilivu. Anavumilia masaibu ya ndoa.
3.     Mwenye mapenzi.
4.     Ni mjinga anaishi katika ndoa kwa sababu ya maeko.
5.     Ni msamehevu anamsamehe mumewe kwa aliyamfanyia.
6.     Ni mwenye kutamani kuishi maisha mazuri.
7.     Mwenye matumaini
8.     Mwenye msimamo thabiti hakutaka kutoka kwa mumewe ingawa alishauri afanye hivyo.

3. SALIM

Ni rafikiye Hamduni.

SIFA

 

1.     Ni mnafiki. Alimwahidi Jamila amuasi duni ili angeweza kutoroka naye.
2.     Ni mwenye mawaidha ya kupotosha. Anamhimiza Jamila atoke kwa duni ili aepuke kuhapo.
3.     Ni msaliti. Anamtaka Jamila ambaye ni bibiye rafiki yako.

4.WANAKIJIJI

1.     Wanapenda amani
2.     Wanamshauri Jamila.
3.       Ni wavumilivu.


4.     SELA

Ni mhusika mkuu anasomea shule ya Askofu Timotheo mwanawe mzee Buteli.
A)    Ana utu na huruma. Hakuavya mimba pia alipokutana na Masazu aliyejifanya  mgonjwa , alimsaidia.
B)    Ni mkarimu. Anampeleka Masazu kwenye kliniki.
C)    Mwenye mapenzi ya dhati.  Anampenda Masazu kwa moyo mmoja anampenda ata baada ya kumpa ua uzito.

MBINU ZA SANAA

Ø  NYIMBO

Mwandishi ametumia nyimbo kwa nia ya kuwasilisha ujumbe Fulani kuonyesha hulka ya mhusika.
Wimbo wa kwanza unaimbwa na Hamduni anapotoka ulevini kuonyesha kuwa hakujali walivyosema wasebuleni.

Ø  MAJAZI

Mwandishi amewapa wahusika majina yaliyolingana na sifa au hulka zao.
Jina la duni halisi lilikuwa Hamduni lakini watu walizoea kulifupisha na kuwa Duni ili litamkike kwa urahisi. Jina hili lilimfanya adharauliwe na watu mtaani sebuleni.
Salim alikuwa rafikiya Duni ambaye aliyejitolea kuleta hali ya utulivu katika maisha ya Jamila kwani alijiona salama na bora kuliko Hamduni.

MBINU ZA LUGHA.

       I.            KEJELI

Duni mtiribu sababu alizoea kuwaamsha majirani zake kwa nyimbo za kilevi. Duni hakuwa mtiribu, hii ni kejeli kwa sababu aliwaudhi wanakijiji kwa nyimbo zake.

2. METHALI

m.f. tunaambiwa kuwa wenyeji wa Sebleni walitoa maneno ya kumlaani Duni akini yalikuwa ni “ dua la kuku haimpati mwewe” yaani Duni, maanake hakubadilika wa kushughulishwa na hayo.

  3. MISEMO

“usiku mkubwa” (uk 66) usiku sana. “ kusafiri kwa mapana na marefu” kusafiri sana. “ mjaliwa laana” mtu aliyelaaniwa.

5.     BALAGHA

Mwisho wa haya utakuwa lini ya Rabi? (uk 67) alijiuliza Jamila hakuwa nalo.

6.     KINAYA

Walimwonea Jamila huruma walisema kuwa huko nje kulikuwa wanaume waungwana na majina na staha zao na ambao wangefanya lolote ili wampate Jamila.

7.     UTOHOZI

Baadhi ya maneno yametoholewa kutoka kizungu ili kuonyesha usasa na pia athari za kizungu kwenye maisha ya wahusika.
k.m: stimu- steam
         Kozi- course
         Bendeji- bandage
         Hai- high
         Dii – dear

8.     TASHBIHI

 Alimpiga mkewe kama ngoma ya kimanga popote apatapo kuonyesha jinsi Duni alivyimpiga mkewe bila huruma.

9.     TAKRIRI

Maneno na semi au kauli zimarudiwa ili kutilia mkazo wazo Fulani k.m mtiribu.

No comments:

Post a Comment