Pages

Mwongozo wa Damu Nyeusi Part 4



KANDA LA USUFI

Hadithi inaanza kwa kisengere mbele kwa kurejelea jambo au tukio lililotokea mwishoni mwa hadithi selaha masazu walikuwa wameenda kumchukua motto wao waliyempata wakiwa bado wanafunzi.
Vijana hawa walikutana wakiwa shule ya upili Sela katika shule ya Askofu Timotheo naye Masaru akiwa shule ya Lenga juu. Urafiki wao unakita mizizi na kupeleka sela kupata mimba na kufukuzwa shuleni.

DHAMIRA

Mwandishi anataka kuonyesha kuwa mzigo wa mwenzioi huwa mwepesi kwako ilhali ni mzito kwake. Wavulana na wanaume watauona mzigo wa kuwa na mimba kama mwepesi lakini kwa wasichana au wanawake mzito.

 

 

MAUDHUI

1.     Mapenzi

Sela na Chris ni wapenzi kwani mapenzi yalishamiri baina yao.

2.     Urafiki

Palikuwa na urafiki baina ya Sela na Chris na baadaye wakawa wapenzi.

3.     Usaliti

Usaliti nni kumtendea mtu jambo kinyume na imani yake kwako. Masazu alimsaliti Sela kwa kutowajibika katika kuchukua jukumu la kumwitikia Sela kwani ni mimba yake.

4.     Elimu

Chris na Sela ni wanafunzi na wanacheza na elimu yao kwa kutotilia maanani shuleni.

5.     Majuto

Babake Sela anajuta kumpeleka Sela shule. Sela na Mavazu wanajuta.

6.     Umaskini

Kwa umaskini, Sela hangepata nguo za kuvalisha kadogo(mtoto) kwani alivalishwa matambara.

7.     Kazi

Chris anapomaliza elimu yake, alienda kutafuta kazi.

8.     Ujanja

Chris anatumia ujanja na kumwambia Sela kuwa ni mgonjwa ili amwongeleshe Sela.

9.     Ndoa

Sela na Chris wanapanga kuishi pamoja.

10.Ushawishi

Sela anamshawishi Chris wamwendee motto wake ili upweke uuondoke.

11.Ukatili

Babake Sela anawafukuza mamake na Sela nyumbani.

12.Ushauri

Mwalimu mkuu anawasihi wazazi wa Sela kumtafutia Sela shule.
Wazee wa jamii wanamshauri babake Sela kumrudisha kwa  jamii zake.

13.Utu

Sela hakuavya mimba.
Razina halati ya Sela anamlisha kadogo.
Sela na mamake walipokelewa na watu wa karibu.

14.Msamaha

Babake Sela aliwarudisha mamake na Sela.

 

 

WAHUSIKA


1.     Sela
2.     Masazu
3.     Kadogo
4.     Rozina
5.     Mzee Butali
6.     Bi. Magret
7.     Mama Sela
8.     Sista
Ingawaje aliweza kuendelea na masomo yake katika shule ya kutwa ya hapo karibu na kwao. Baada ya kujifungua alikaa nyumbani kwa miezi mitatu akikitunza kitoto chake. Baadaye alimwachia mamake na kurudi shuleni.
Baada ya masomo yake Masazu, alihamia mjini Dafina kutafuta kibarua, na kupata cha kuvuna mkonge upweke na akaonolea kuwa jambo la busara kama angekuwa na mwana wo, kadogo ili amtoe apweke wakati Masazu akiwa kazini.
Sela na mchumbaye waliamua kumwendea mwanao hadi kule kijijini alimokuwa akikaa na halati ya Sela, walipanga safari yao usiku na ikatokea kuwa kulikuwa na mvua iliyosababisha unyevu na utelezi. Walipokuwa njiani wakirudisha Sela na mtoto mgongoni, aliteleza na kuanguka kwenye mto uliokuwa umefurika na kusombwa na maji pamoja na mwanao kadogo.
Masazu alipoona hivyo alijitosa majini ili kuwaokoa. Hadithi hii inapoishi hajabainika kama Masazu aliweza kuwaokoa . Hadithi hii inapoisha hajabainikakama Masazu aliweza kuwaokoa au labda pia alisombwa na maji. Hadithi inaisha kwa taharuki.

 

 

MBINU ZA KISANAA

Ø Mbinu rejeshi
Ø Taharuki
Ø Maswali ya balagha
Ø Taswira
Ø Sadfa

1.    Mbinu rejeshi

Hadithi inahusu kumwiba motto lakini mwandishi atarejesha nyumba vile walivyopatana.

2.    Maswali ya Balagha

Haya ni maswali ambayo hayahitaji majibu. K.m mama Sela aliuliza Masazu, “ huyu si mtoto wetu sisi wawili?”
Bw. Butali aliuliza,” mama gani anayemtazama mwana akigeuka afriti?”

3.    Taswira

Hii ni picha ijengewayo mawazoni. K.m. Masazu anachomeka kidole chake ardhini na kula kiapo cha mapenzi yake kwa Sela.
Masazu akiweka vidonge vya dawa kwa mdomo na kumeza kwa maji.

4.    Taharuki

Mwandishi anatueleza kuwa Masazu anapokula kiaop nakiwiliwili cha Sela kinalengezwa na mengine yaliachiwa yalibaki katika himaya ya maumbile.

5.    Sadfa

Sela na Masazu walikutana bila kutafutana na baadaye kuoana.
Bw. Butali hakutarajia mambo aliyokumbana nayo yafanyike kwake.

 

Christine

MBINU ZA KISANAA

1.Mbinu rejeshi.
-Hadithi inahusu mapenzi ya Sela na Masazu.
-Mwandishi anaturudisha nyuma mahali ambapo Masazu na Sela walikutana.
2.Maswali ya balagha.
-Mamake Sela anamuuliza babake Sela kwani Sela si msiba wao bali wa mamake tu.
-Masazu anauliza Sela kwa nini hakujikinga.
3.Taswira.
-Hii ni picha ya mawazoni.
-Hii inajitokeza ambapo Masazu anakichomeka kidole chake ardhini akiwasilisha kiapo kwa Sela kuwa mapenzi yake ni ya dhati.
4.Taluki.
-Hali ya kutojua kilichotendeka hapo mbeleni.
-Ambalo Sela na mtotowe wanatumbukia majini.
-Wakati ambapo Masazu aliapa kiapo aliyeyusha nafsi ya Sela na hatukwambiwa nini ilitendeka.
5.Sadfa.
-Haya ni mambo ambayo hayakutarajiwa kutendeka.
-Sela na Masazu walioana hata baada ya Masazu kumsaliti.

MBINU ZA LUGHA


1.TASHBIHI

Hulinganisha kitu na kingine k.m;
·        Kiwiliwili chake mithili ya mbwa anayekabiliana na chatu macho kwa macho.
·        Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaendaarijoyo.
·        Nafasi kama hiyo hutokea kwa nadra ya jua kupatwa na chui aliyelivizia windo lake na sasa limetokea, akajiandaa.

2. Tashhisi

Sifa ya kukipa kitu chenye hakina uhai( uhaishi)
·        Mambo haya mawili yalielekeaa kuungana kuhujumu mkakati wao.
·        Matone yalitua sehemu yao ya hujuma. Mwandishi arejelea pale ambapo Sela na Masazu walikuwa wamejificha chini ya mwembe.
·        Mabaki yalielekea kutapika wanafunzi wakikena kiume.

3.Semi.
·        ….baridi shadidi ya usiku(uk59)ina maana kuwa huo ulikuwa na baridi kali.
·        Alijaribu kuvuta kumbukumbu(uk59)yaani alianza kukumbuka.
4.Methali.
·        Mimba ile ya Masazu ilikuwa kanda la usufi.Methali hii inasema kuwa mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
·        Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.(uk63)
5.Istiara.
·        Nyumbani mwa Butali kuligeuka kuwa jehanamu.
·        Mimba ya Sela inalinganishwa na msiba.
·        Usiku wa giza-kukosa matumaini.






               
SHAKA YA MAMBO.
 Hadithi hii inamhusu msichana  wa miaka 29 hivi.Tunampata asubuhi na mapema akiwa mwenye gari la abiria akielekea kazini.Anapata gari limejaa lakini kijana mmoja anamwondokea kiti ili akae,jambo lisilo la kawaida hasa hapa Afrika.Akiwa njiani anawaza mengi kuhusu maisha yake.Anaona kuwa tangu afike Nairobi hajapata yale mambo mawili aliyoyafuata kujifunza usekritari na kuwa na uhuru.
Alikuwa anaishi na mzee Mwinyi  na familia yake katika mtaa wa Madaraka Estate alipokuwa amekodisha nyumba.Mzee huyu alimchukua kama mwanawe.Pia alikuwa na rafiki wa kiume aliyeitwa Kamata.Hatimaye anafika kazini,mkahawa uliokuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K.I.A na kuanza kazi.Mkubwa wake Grace hangeweza kushika zamu yake kwa sababu alikuwa na miadi yake lakini angemlipa baadaye.Kamata alifanya ya kukagua ya wasafiri humo uwanjani.
Tunamuona mzungu mteja akiacha bunda la noti za dola ya Kimarekani  zaidi ya alfu moja.Esther anachukua na kushindwa atazipeleka wapi.Kisha Kamata na Grace wanaingia na kuanza kuchukua  zile dola Kamata akidai kuwa atampa mwenyewe pesa.Ajabu ni kuwa Kamata hakumwona yule mzungu tena.Angemjuaje?Kisha Esther na Kamata  walikuwa wakisuhubiana.Esther akawaza kuwa Kamata hawezi mjua abiria huyo kwani hakumweleza wasifu wake.

Maudhui.
                              Ni adhali ya maisha ya mjini hasa kwa vijana watafutao kazi.
Kazi.
Tunamuona Esther akielekea Nairobi kutafuta kazi.

Unafiki.
Kamata anajifanya mwema na kuchukua zile pesa na hajui anayempelekea.

Uaminifu
Esther anaaminika kwa kazi yake.

Elimu.
Esther amesoma na bado anataka kuendeleza masomo.

Shaka(kukosa uhakika)
Esther anashaka kuwa Kamata atarudisha zile pesa.

6 .Usasa na mabadiliko.
Zamani wanawake hawakuelimishwa  lakini swala hili limeingia ambapo Kamata anampisha Esther kiti kwenye gari.

7.Uajibikaji.
Esther aliwajibika kazini mwake.

8.Uvumilivu.
Esther anavumilia akidhani atabadilishwa zamu.

9.Usaliti.
Grace  anamsaliti Esther kwa kuwa na uhusiano na Kamata.

Wahusika.
1.Esther.
-Ni mhusika mkuu.
-Ametoka Machakos.
-Anafanya kazi ya hoteli J.K.I.A
-Anaishi kwa mzee mwinyi.

Sifa.
1.Mwajibikaji.
Aliajibika kwa kazi yake katika hoteli.
2.Mshamba.
Anadanganywa kwa rahisi sana. 

3.Mvumilivu.
Alisubiri ili abadilishwe zamu.

4.Mwoga.
Hakutaka kuambia Kamata anampenda.

5.Mwenye shaka.
Alishaka kwa vile pesa zitamfikia yule mzungu.
6.Mwadilifu.
Hajiingizi katika mapenzi ya nje ya ndoa.
7.Mwenye mapenzi ya dhati.
Anampenda Kamata.
8.Mwaminifu.
-Alipopata zile dola alimrejeshea mteja.
-Anashawishika kwa urahisi.

2.Kamata.
-Ni mfanyikazi katika uwanja wa J.K.I.A
-Ni rafikiye Grace.
-Anapenda starehe na anasa.
Sifa.
1.Ndumakuwili.
-Ana uhusiano na Grace na Esther.
2.Mlaghai.
Anamdanganya Esther.
3.Msaliti.
Anamsaliti Esther mapenzi yake.
4.Hana subira.
Aliona gari la Esther limekaa na kuingia kwa Grace.

3.Grace.
-Ni rafikiye Kamata.
-Ni mkubwa wa Esther kazini.

Sifa.
1.Mpenda anasa.
Anaenda vilabuni kisiri na Kamata.
2.Msaliti.
Anamsaliti Esther.
3.Mwenye tamaa.
Anatamani bunda lile na dola la mzungu.
4.Msiri.
Hakumweleza Esther  wanaenda na nani.
5.Mwongo.
Wana uhusiano na Kamata na kumdanganya ya Esther kuwa hawana uhusiano na Kamata.
MBINU ZA LUGHA.
1.Maswali ya balagha.
Kuna maswali ya kuchochea hisia na ambayo hayana majibu.kwa mfano.
Esther anapokuwa kazini anawaza sana kumhusu Kamata.Anajiuliza maswali ya balagha kama Kamata kweli anamjali naye huyu pia anashughulika kutafuta pesa.
2.Utohozi.
Baadhi ya maneno ya kizungu yametamkwa kama ya Kiswahili.km kompyuta-computer,disko-disco,blauzi-blouse.
3.Mbinu rejeshi.
Inatumika katika (uk4) ambapo mwandishi anaturudisha nyuma katika maisha ya babake Esther.
4.Tashhisi.
Hali ya kuvipa vitu visivyo hai sifa za vitu vyenye uhai.



NDOA YA SAMANI





Hadithi hii inasimuliwa katika nafsi ya kwanza.Mwandishi amechukua nafasi ya mhusika mkuu,Abu na kumtumia kusimulia.Hadithi inaanza kwa kisegere nyuma.Mbele kwa sababu msimulizi anaanza kwa sehemu inayopaswa kuwa ndiyo ya mwisho wa hadithi.
Abu anaeleza kuhusu harusi iliyokuwa ikifanyika kati yake na Amani.Mwanzoni Abu alitaka kumuoa Amali lakini kwa kuwa alikuwa maskini wazazi wa amali wakakataa.Baadaye alipata kazi ya uhamali Arabuni na kuweza kujiwekea akiba iliyomsaidia kuanzisha biashara ya uchukuzi  wa abiria na kutajirika sana.
Kwa kuwa  hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana yeyote,marafiki zake walimshauri  amrudie Amali wake.Abu alirudi kwa akina Amani ili kumposa tena safari hii lakini wazazi wa Amali hawakumkatalia posa yake hasa kama ilivyokuwa desturi yao.Wazazi wa Amali walimshauri Amali  aagize kununuliwa zawadi tele na za bei ghali na Abu.
Ikawa pia harusi sharti ifanyiwe nyumbani mwa Amali na tena iwe kukata na shoka.Siku ya arusi ilipofika kila kitu kilikuwa shwari lakini Abu alikataa kushiriki katika awa hii na hivyo basi arusi ikavunjiliwa bali.Abu alisihi kuwa Amali hakumpenda yeye bali aliyapenda mali aliyonayo sababu ya Abu kufikiri hivi ni kuwa sababu Amali alikuwa amemkataa alipokuwa maskini.Harusi iliyotarajiwa haikutendeka bali iliwaacha watu vinywa wazi. 
Dhamira.
Ndoa  yapaswa kujengwa katika msingi wa mapenzi si wa mali.Mwandishi anataka kutufundisha kuwa ndoa nzuri si ya pesa.

Maudhui.
1.Ndoa.
Msimulizi alimtaka Amali amwoe lakini kulikuwa na katizi kwa upande wa mvulana kwa kuwa hakuwa na pesa.Inatufunza usiolewe kwa sababu ya mali.Ndoa iwe ni maamuzi ya wenye kuoana.
2.Umaskini.
Msimulizi alikuwa ametoka kwenye familia ya kupigiwa mfano.Mwandishi anazingatia swala la umaskini lisiwe zingitiki kwa mapenzi.
2.Tamaa.
Mamake Amali alikuwa na tama ya kutajirika ndio maana alimkataa mwandishi mwanzoni.
4.Kisasi.
Msimulizi alilipiza kisasi kwa kukataa kumwoa Amali kwa vile yeye alikahaliwa mwanzoni.
5.Usaliti.
Amali alisalitiwa na msimulizi aliyemtoroka siku ya arusi.Mamake Amali alimsaliti mwandishi kwa kumkataza mwanzoni aoe Amali.Pia alimsaliti Amali kwa kumkataza aolewe na mwandishi.
6.Changamoto.
Mwandishi anapitia mambo magumu .mfano;Umaskini,kukosa kazi na pia kukataliwa na mamake Amali.
7.Bidii.
Mwandishi  alienda Arabuni na kujikaza na kuwa tajiri.
8.Utajiri.
Mamake Amali anataka kutajirika.

Wahusika.
1.Mwandishi.
Ni mhusika wa kiume anayopitia mambo magumu maishani.
Sifa.
1.Mchochole.
Kwao walikuwa maskini wa kupigiwa mfano.
2.Mwenye bidii.
Alipopata uajiri Arubani, alitia bidii na kutajirika na kuweza kujenga nyumba yake pamoja nay a wazazi wake.
3.Msaliti.
Alimsaliti Amali kwa kukosa kumuoa.
4.Mwenye kisasi.
Alikataa kumuoa Amali kwa vile alikataliwa hapo zamani kumwoa na Mamake Amali kwa kuwa hakuna na pesa.
5.Mkarimu.
Aliitikia kununua vitu ambavyo alivyopendekezwa kununulia familia yake Amali ili amuoe.Pia aliwatafutia ndugu zake kazi huko Arabuni.
2.Amali.
Msichana aliyetakiwa kuolewa na msimulizi.
Sifa.
1.Mtawa.
Anakaa kwao nyumbani na kutojishughulisha kwenda kufanya mapenzi kiholela.
2.Mtiifu.
Anawatii wazazi wake na pia dini yake.
3.Mrembo.
Wengi walimtaka kwa sababu ya urembo mwandishi aliyesoma.
4.Mtamaduni.
Alifuata mambo ya kitamaduni.
3.Wazazi wa Amali.
(i)Mamake.
Sifa.
1.Mwenye tamaa.
Anaitisha mahali ya bintiye ili atajirike.
2.Mwenye ubinafsi.
Anajiitishia vitu vyake pekee kama mahari ili Amali aolewe.
Mtindo wa lugha.
Ametumia misemo .kwa mfano;
Kupata jiko-kuoa
Walalahai-tajiri
Walalahoi-maskini
Maskini hohehahe-umaskini



MIZIZI NA MATAWI


Hadithi hii inatusimulia kisa cha mvulana mmoja kwa jina lake Sudi.Alilelewa na mama tajiri aliyemsomesha hadi chuo kikuu na mwishowe akaajiriwa.Alizoea kuuliza kama alikuwa na babake mzazi tangu utotoni akajulizwa kuwa babake mzazi ni Abdalla lakini hajawahi muona.
Siku moja alimuuliza mamake aliyetengeneza hadithi ya uongo kuwa Abdalla alimkimbia akiwa bado hajamzaa Sudi.Jioni moja Sudi akitoka stareheni zake alikutana na mwanamke mmoja aliyemwomba usaidizi.Alimpeleka  hadi kwao na kumwajiri kama yaya.Bibi huyu alimsimulia  Bi.Mkubwa jinsi alivyomtupa mtoto kwenye pupa la taka kwa kukosa uwezo wa kumlea.
Baadaye Bi.Mkubwa alimweleza Sudi kuwa mamake mzazi ni yule mfanyikazi wake na kuomba wasameheane.
Dhamira.
Hadithi hii inatufunza kuwa hata mtu akipotelewa na waliokaribu naye ama wakose kumsaidia bado anaweza kuendelea na kufaulu maishani.
Maudhui.
1.Mapenzi.
Sudi alipendwa na wasichana wawili Radhia na Waridi.Wasichana wengine pia walimpenda  Sudi kwa  utanashati wake.
2.Ukatili.
Bi.Kudura alifanya ukatili kwa kumtupa mwanawe kwenye pipa la takataka.Alijua hili lilikuwa kama kuua lakini hakujali.
3.Majuto.
Bi.Kudura anajuta kwa kumtupa mwanawe na baadaye hakuweza kupata mtoto aliomba Mola amsamehe.
4.Uana haramu/malezi.
Sudi hakumjua babake jambo lililomsumbua sana kimawazo.
Alimuomba mamake amwambie ukweli lakini alimdanganya.
5.Elimu.
Licha ya kuwa mwanaharamu,Sudi alisomeshwa na mamake hadi kiwango cha juu hadi akawa daktari.
6.Anasa.
Sudi alipokuwa ulaya alihudhuria sherehe iliyokuwa ya kukata na shoka ambayo ilikuwa ni sikukuu ya pasaka.Kulikuwa na muziki na wanawake wengi walitaka kucheza na Sudi.Pia alimpeleka mpenziwe Radhia kustarehe huko.
WAHUSIKA.
1.Sudi Abdalla.
(a)Mtana shati.
Ni kijana aliyependa usafi sana kwani tunamwona akijikwatua alipokuwa akijiandaa kwenda karamuni.
(b)Mkarimu.
Mara kwa mara alimpata Bi.Kudura njiani na hakumpita .Alimpa msaada aliotaka.
(c)Mwenye heshima.
Aliwaheshimu mamake na Bi.Kudura .Licha ya kuwa Bi.Kudura alikuwa maskini mwombaji,Sudi alimwita kwa majina ya heshima.Pia hakuwahi kumtuma amletee chochote.
(d)Mwenye utu.
Kutokana na utu wakealimsaidia Bi.Kudura.Alimwonea huruma alipompata njiani karibu na makaburi.
(e)Anapenda anasa.
Anapenda kuhudhuria karamuni na sherehe na mpenziwe Radhia.
(f)Mwenye mapenzi ya dhati.
Alimpenda sana mamake na Radhia mpenziwe na kufanya uchumba naye.

2.Bi Mkubwa.
Huyu ndiye aliyemwokoa Sudi alipotupwa kwenye pipa la takataka na mamake mzazi.Alimlea kama mwanaye.
Sifa zake.
1.Ni mwongo.
Alimdanganya Sudi kuwa yeye ndiye mamake mzazi  na kuwa babake alikuwa akiitwa Abdalla lakini alikufa na kumwachia mamake ulezi.
2.Ni mkarimu.
Bi.Kudura alipopelekwa kwake alikubali kukaa naye na hata akampa vitu alivyoagizwa na Sudi.
3.Ni msiri.
Aliweza kuiweka siri juu ya asili ya Sudi kwa muda mrefu tangu Sudi akiwa mtoto.
4.Mwenye mapenzi ya dhati.
Bi Mkubwa alimpenda Sudi na kumlea kama mwanaye.
5.Msamehevu.
Alimsamehe Bi.Kudura naye akasamehewa na Sudi.

3.Bi.Kudura.
Huyu ndiye aliyemzaa Sudi nje ya ndoa na kumtupa kwenye pipa la takataka kwa sababu aliona aibu.
Sifa zake.
(a)Ni mkatili.
Alifanya ukatili kwa kumtupa mtoto mchanga kwani hakujua kama angeokotwa na mtu au angeliwa na mnyama.
(b)Ni mnyenyekevu.
Kwa sababu ya hali yake ya umaskini alinyenyekea ili asaidiwe.
(c)Ni mcha mungu.
Alijua kuwa tendo la kumtupa mwanawe ilikuwa dhambi kwa mungu.

MBINU ZA SANAA NA LUGHA.
1.Taharuki.
Sudi alikuwa na hamu ya kumjua babake mzazi.Naye mamake alimweka na taharuki kwa muda mrefu.
2.Methali
-Mungu akikupa kilema hukupa na mwendo.Sudi alitaka mamake amwambie ukweli ndipo ajue jinsi ya kuishi na ukweli huo.
-……yaliyopita huwa yamepita.Sudi alitaka kuyasahau maisha ya anasa aliyoishi alipokuwa ulaya.
-Kuvyaa kupona.Mwanamke anapopata mtoto,mtoto huyo atakuja kumfaa baadaye akiwa mkubwa.
-Damu ni nzito kuliko maji.Bi.Kudura aliongozwa na kudura hadi ilipo damu yake na kumpata mwanawe Sudi.
3.Misemo.
-Kata tama-kosa matumaini.
-Tulia kama maji ya mtungi-tulia sana.
-Piga gari moto-Gurumisha gari.
-Walikuwa hawajijui hawajitambui-hawajiwezi.
-Piga moyo konde-Amua kufanya jambo.
4.Maswali ya balagha.
-Furaha yangu itoke wapi tena?
-Kuna ukatili gani zaidi ya huo?
5.Kuchanganya ndimi.
Kwa mfano:Handsome,Tea breeze,Royal palm.
6.Uzungumzi nafsia.
Sudi alijisemea mwenyewe anaposema.’Kumbe ni kweli  wanavyoniita’Sudi alisaini kimoyomoyo.
7.Tashhisi.
Gari unahaishwa tunapoambiwa kuwa Sudi alipiga gari lake moto na taratibu likatambaa na kuanza masafa kuelekea lilikokusudiwa.
8.Jazanda.
Kwa Sudi maneno haya yalikuwa msumeno unaokeketa kwa maumivu makti.
9.Tashbihi.
…..lakini ulimi wangu mzito kama nanga.
10.Mbinu rejeshi.
Sudi anaturejesha nyuma huko ulaya  alipokuwa akisomea na kutuonyesha jinsi maisha yalivyokuwa.
11.Sadfa.
Kukutana kwa Sudi na Bi. Kudura ilikuwa sadfa kwani hakutarajiwa.
12.Utohozi.
Hoteli-hotel
Bia-beer
Muziki-music
Benki-bank
Densi-dance
 13.Nidaa.
Sudi alikuwa akitabasamu-tabasamu ya fahari kwa uzuri wake.
Alifariki ghafla na kuniacha na mimba yako,tena changa!
Ikawa kama mtu aliyefundua tandu akafundika nge.
Naam,watu walikuwa wawiliwawili…ndume na mke!
Alimrudi  kila mmoja alikuwa na ulimwengu wake.
Inanikumbusha kauli ya wahenga …kuvyaa kupona!
Aa vile nao na umetulia! Hapo kabsa!

Mwongozo Wa Damu Nyeusi Part 1


 MKE  WANGU


                             Hadithi hii inaanza wakati ambapo msemaji alikuwa anachaguliwa mke atakayeoa na wazee wake lakini hakutaka hivyo yeye alimtaka motto mbichi ambaye angemvumbika mpaka aive. Pia alimtaka mke ambaye alikuwa na sifa ambazo angetaka mke wake awe nazo. Alimweka Aziza rohoni mwake kwani alikuwa kinyume na wasichana ambao walikuwa wamesoma. Alikwa amesoma skuli akapata kuwa mjuaji sana. Msemaji anasema kuwa alipomaliza masomo yake ya juu,mamake alianza kumshawishi  kuhusu mambo ya ndoa. Mama alimtajia wasichana kadhaa lakini aliwakataa wote  na kusema kwamba alimtaka Aziza aliamua kumwoa.
        Baada ya harusi na sherehe walienda fungate yao ambapo msimulizi alipata kumsoma Aziza  na apate kumsomesha. Katika harakati ya kumsoma Aziza,msimulizi aliona kwamba Aziza hakuwa na mazungumzo pamoja naye ,pia aliona jinsi alivyokuwa akimtazama kwa unyarafu. Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo,alisema kuwa alimsikitikia kwani alimwona kama gumegume tu wala si mume wake  kwa sababu hakuwa anafanya kazi yoyote isipokuwa kutembea tembe.
       Aziza aliteta pia kwamba mumewe alikuwa na mikono laini kiasi cha kuwa angemguza mwanamke hangehisi chochote. Aziza hakuwa anavalia viatu kila alipokwenda, na alipoulizwa mbona havalii alisema kwamba hataki kutegemea ngozi za ng’ombe aliyekufa .
     Msimulizi anasema kwamba  humwamrisha mkewe atakavyo kutamshinda. Pia anasema kuwa anaona fedheha kuu,kwanialio  kisonoko ambaye hangeweza kutoka  naye  mbele za watu  alishangaa  jinsi atakavyoishi  naye mbele za watu. Alishangaa jinsi atakavyoishi naye kwa sababu hata mambo madogo ambayo ni muhimu hatilii maanani.
    Aziza alikuwa amenunuliwa brushi ya meno na dawa ya meno lakini hakuvitumia hata kidogo.Aliamua kumuuliza asili yake.
    Msimuluzi alipomuuliza kwa nini hakutumia brushi Aziza alisema kwamba ana mswaki  wake binafsi ambao ulikuwa  umetengenezwa  na mnazi na ndani mlikuwemo unga uliokaa kati kati baina ya jivu na masizi. Aziza alisema kuwa hatautia mswaki ule mdomoni ati kwa sababu  na manyoya ya nguruwe. Pia alisema kuwa wanaotumia brashi baada ya miezi matatu ama mitano huenda kumwona daktari wa meno.
     Siku hiyo, Seluwa mtoto wa shangazi yake aliwatembelea. Wazee wa msimulizi walitaka amwoe Seluwa lakini alimkataa kwa sababu zake. Seluwa na Aziza walikuwa wakitaniana ‘mke mwenzangu’ na pengine ‘wifi yangu’. Wakiwa katika mazungumzo yao Aziza alismskia Bazazi wa madafu akipita huko nje. Msimulizi alimpa Aziza shilingi mbili akanunue hayo,kasha Aziza akamwita Bazazi huyo aende nyumbani mwao.
Bazazi huyo alipofika humo, Aziza akamwambia bwanake kwamba nia ya kumwita huko nyumbani ilikuwa ili aone kuwa alitaka bwana kama huyo. Hayo  ni kwa sababu daima alikuwa anafikiri kazi tu. Baada ya kumwambia hayo,Aziza alimwambia bwanake aampe talaka yake.

2.    Wahusika
Hadithi hii ya Mke Wangu ina wahusika wafwatao;
Msimulizi
Aziza
Fedhele Salim
Salma
Seluwa
Wazazi wa msimuliza
Wahudumu wa msimulizi k.v Mapanya
MSIMULIZI
Msimulizi ni mhusika mkuu katika hadithi. Alizaliwa katika familia ya kitajiri kama anavyotueleza katika ukurasa wa 18.. Ni kijana wa kisasa na mumewe Aziza.
Ni mtamaduni kwa sababu anautii utamaduni wa jadi unaompendelea mwanamume.
Yeye ni msomi aliyesoma hadi viwango vya juu vya elimu.
Aidha, msimulizi anaweza kuelezwa kama mzembe kwa sababu hataki kujihusisha na kazi za sulubu kama vile kuangusha nazi, kuchoma na kuuza mihogo pamoja na kazi nyinginezo. Anashangazwa na uamuzi wa mkewe wa kutotaka kufuliwa nguo wala kuooshewa vyombo.
Ingawa tumemtaja kama mtamaduni, Msimulizi anaweza kueleweka kama mwanausasa kwa sababu anampendekezea mkewe kutenda mambo ya kileo kama vile kuvaa viatu na kupiga mswaki. Kwa sababu hii, anadhihirisha tabia ya mtu asiye na msimamo dhabiti. Ukosefu huu wa msimamo unamfanya ashindwe kujiamulia mambo muhimu maishani kama vile; mke wa kuoa, kazi ya kufanya na namna ya kuiongoza familia yake changa. Kwa maneno  mengine, msimulizi ni mhusika aliyekengeuka na asiyejifahamu.
Isitoshe, msimulizi ni mvumilivu na mwenye subira kwa vile si mwepesi wa kutibukwa na hisia tunadhihirishiwa kuwa anamvumilia Aziza kama mkewe licha ya fedheha anayoipata mbele ya wageni wao wenye ustaarabu wa kimjini. Licha ya Aziza kumdharau, kumwita gumegume na kumsuta kwa kutofanya kazi maishani, msimulizi haonyeshi kuudhishwa na mkewe.
Badala yake, msimulizi anamkubali na kumvumilia mkewe akitaraji kuwa siku moja atazinduka na kuukumbatia usasa na ustaarabu. Aziza anafikia kiasi cha kumwita bazazi wa madafu kasrini mwao, kumsifu bazazi wa madafu mbele ya mumewe na hata kumuomba mumewe talaka. Msimulizi haonyeshi kukasirishwa na maudhi haya yote.
Ni mwenye taasubi ya kiume; hulka hii inadhihirishwa pale ambapo anatarajia kumpata mke ambaye hakwenda skuli. Nia yake ni kumpata mke ambaye hatakuwa katika ngazi moja ya kielimu naye. Tunaweza kuhitimisha kuwa msimulizi hataki mwanamke mwenye ung’amuzi wa usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kwa  mujibu wake, matatizo ya ndoa hutokana na midomo na ujuaji wa wanawake.
Aidha, anapanga kumvinya mkewe na kumfunza mambo ya kisasa ya uanagenzi. Anammithilisha mkewe na tunda linalohitaji kuvinywa. Anaonyesha dharau kwa wanawake kwa sababu anawalinganisha na watoto wadogo ambao hawaachi kisebusebu (uk. 21)
Umuhimu wa msimulizi
Msimulizi ni mhusika mkuu katika hadithi hii. Anaakilisha kizazi kilichochanganyikiwa. Kizazi kilichojipata katika nja panda, yaani katikati ya ukale na usasa.
Mbali na kuchanganyikiwa, msimulizi anaakilisha matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii ya kisasa kama vile mfumo mbaya wa elimu inayolenga ajira, ukosefu wa ajira, ujuma na uzembe, matatizo ya ndoa na kadhalika.
Msimulizi ni kielelezo cha jamii ambayo inashindwa kuyaelewa mazingira yake. Anashindwa kuuelewa utamaduni wake, mahitaji yake majukumu yake, na hata hamwelewi mkewe.
Waama, ni kupitia kwa mahusiano ya Msimulizi na mkewe ndipo tunabaini kuwa elimu na hekima ni mambo mawili tofauti.

AZIZA
Ni mhusika mwingine ambaye anaweza kuutajwa kama mhusika mkuu. Ni mkewe msimulizi. Tofauti na msimulizi, Aziza alizaliwa na kukuzwa shamba.
Aziza ana sifa zifwatazo;
Kwanza, Aziza ni mdadisi wa mambo. Anamchuja msimulizi na kuugundua udhaifu wake. Ni kutokana na udadisi huu ndipo anagundua kuwa yeye na msimulizi wako na mawazo yaliyobaidika.
Anaumaizi ulelemama wa mumewe wa kutofanya kazi na tabia ya kutegemea wazazi wake. Anadadisi na kugudua viungo vya dawa ya meno; tumbawe, sabuni na arki za peremende kali. Pia, anagundua kuwa mswaki si lolote si chochote bali nywele za nguruwe.
Aziza anaweza kuelezwa kama mhafidhina, anayapinga madai ya msimulizi kwamba riziki ya kazi imekosekana. Yeye anashikilia kuwa mtu hawezi akakosa kazi ulimwenguni, kazi anazozitaj ni kazi za jadi kama vile kuangusha nazi, kuchoma na kuuza mhogo na hata kuchunga punda. Uhafidhina wa Aziza unazidi kujiidhihirisha pale anapokataa katakata kuvaa viatu huku akishikilia kukanyaga chini kote aendako. Anawadharau wanaume wa kimjini enye usasa na mwishowe anajiafadhalisha kuolewa na mwanamume wa shamba.
Mwenye dharau; kila mara, Aziza anamchuja mumewe kwa dharau. Anavidharau viatu, mikono ya mumewe, mswaki na dawa ya meno ya kisasa. Kitendo cha kumsifia bazazi wa madafu mbele ya msimulizi pia ni ishara ya dharau.
Sifa nyingine ya aziza ni kuwa yeye ni mwenye hekima, majibizano yake na mumewe yanadhihirisha hekima tele. Anashangaa ni kwa nini walishwe na wazazi wa msimulizi. Anaumaizi udhaifu uio kwenye dawa ya kisasa ya meno, anashangaa ni kwa nini wale waliotumia dawa ya meno waliyang’oa meno yao kila wakati. Hekima hii inamfanya msimulizi kukiri kuwa mkewe ni mtu asiyeweza kupatwa kiotoni.
Mwenye msimamo thabiti; Aziza anadhihirisha kuwa na msimamo thabiti kwa mambo anayoyaamini. Anakataa kushawishiwa kuukumbatia usasa. Anashikilia na kuyaishi maisha ya jadi hata kama kila mtu aliye karibu naye ameukubali usasa.
Anapojibizana na mumewe, Aziza anajitokeza kama mhusika jasiri. Anakataa kuwekwa chini na mumewe. Hali ya kutopata masomo ya kisasa haimnyimi uasiri wa kuaimama kidete na kuyatoa mawazo yake. Kutokana na ujasiri wake, anamkabili mumewe na kuzishutumu tabia zake bila hofu wala woga. Hatimaye, anamjulisha msimulizi kimasomaso kuwa angetaka apewe talaka yake.
Umuhimu wa Aziza
Aziza amechorwa kama mhusika bapa sugu. Anao msimamo sugu kuhusu utamaduni wa jadi na hakubali kuubadili msimamo huu.
Anawakilisha watu wanaoshikilia msimamo thabiti wa kuutetea ujadi. Aziza anaweza kutazamwa kama mdomo wa mwandishi kwa sababu mwandishi amempa hekima nzito na amewezeshwa kumpiku msimulizi katika migogoro yao mbalimbali.
Aidha, aziza ametumiwa na mwandishi kuutetea utamaduni wa waafrika dhidi ya athari za kigeni kama vile elimu na mavazi.
Aziza ametumiwa kupitisha ujumbe kuwa furaha na utu wa mtu si elimu wala utajiri wala ajira, bali maadili mema, bidii, heshima na mapenzi ya dhati.
Kupitia kwa Aziza, tunajuzwa kuwa mwanamke wa kiafrika amejikomboa kimawazo na anaweza kujifanyia maamuzi tofauti na adhaniwavyo na wanaume wenye taasubi za kiume kama msimulizi.
Maswali
1.      Jadili uhusika (hulka na umuhimu) wa msimulizi na wa Aziza
2.      ‘Msimulizi na mkewe hawapatani kwa lolote’, jadili kauli hii ukirejelea hadithi fupi ya Mke Wangu.
FEDHELE SALIM, SALMA NA SELUWA wanaweza kuelezwa kama wasichana wa kisasa; msimulizi anawataja kama wasichana waliojaa utamaduni wa kisasa.
Fedhele anaelezwa na msimulizi kama msichana msomi. Ingawa hivyo, tabia yake ya kuvalia kanzu fupi na kuandamana na wanaume hazimpendezi msimulizi.
Salma anadhihirika kama msichana mwenye kujipodoa na marangi ya mashavu na midomo.
Msimulizi anatueleza kuwa Seluwa ana ‘kidomo’ yaani, ni mtu wa kuongea maneno mengi. Isitoshe, katika uk. wa 24, anamtaja Seluwa kama msichana mwenye kujipodoa na kupendeza.anamtaja kama mwingi wa bashasha, mizaha na furaha.
Umuhimu wa Fedhele, Salma na Seluwa
Hawa watatu ni wahusika wasaidizi.
Wanatusaidia kumwelewa msimulizi kwa sababu wanatusaidia kujua ni mambo gani yasiyompendeza msimulizi.
Aidha, sifa zao zinakinzana na za Aziza hivyo basi wanatusaidia kujua hulka za Aziza.
WAZAZI WA MSIMULIZI ni wakwasi kwa sababu msimulizi anatueleza kuwa yeye alizaliwa katika familia ya kitajiri.
Wao ni wahifadhina kwa sababu wanamlea mtoto wao kwa kuongozwa na tamaduni za jadi za kiafrika na hata wanamchagulia mke kwa mujibu wa kaida za jadi za kiafrika. Msimulizi anatueleza kuwa, …wazee wangu, juu ya utajiri wao, hawakupenda kubadili mila zetu… (uk. 18)
Mamake msimulizi anadhihirisha hekima anapomwongoza msimulizikumchagua na kumwoa Aziza. Anapendekeza wasichana ambao anajua msimulizi hatakubali kuwaoa.
Umuhimu wa wazazi wa msimulizi
Wazazi wa msimulizi ni wawakilishi wa utamaduni wa jadi.
Maswali
1.      Jadili uhusika wa msimulizi na Aziza
2.      Je, Seluwa, Salma na Fedhele Salim wana umuhimu gani katika hadithi
3.      Unadhani ni kwa nini mwandishi akatumia anwani ya mke wangu
4.      Ni vipengele vipi vya utamaduni wa jadi anavyovipendelea mwandishi.

3.    DHAMIRA
Yaelekea kuwa mwandishi ana nia ya kutubainishia kuwa Elimu ya jadi ni bora kuliko mafunzo ya kisasa ya shuleni na vyuoni; hili linabainika tunapoona Aziza akipewa sifa ya kuwa mpevu wa hekima nzuri na mwandishi.
 Msimamo wa mwandishi ni kuwa watu wa shamba waolewe na wenzao wa shamba na wale wa mjini waolewe na wale wa mjini. Msimamo huu umetokana na yale anayoyaona katika jamii; migogoro katika ndoa, ubaidi wa kifikra utabaka na mitazamo ya maisha inayokinzana.
Yamkini wimbi la kisasa ambalo limeiacha jamii ya kisasa katika njia panda limemchochea mwandishi kuiandika hadithi hii ili awakumbushe watu kurejelea kaida zao za jadi.
4.    MAUDHUI
Mafunzo yafwatayo yanajitokeza katika hadithi ya Mke Wangu.
·         Utamaduni
·         Usasa na mabadiliko ya kijamii
·         Elimu
·         Utabaka, utengano na mitafaruku
·         Ndoa
·         Taasubi ya kiume na matatizo yanayowakumba wanawake
·         Ukengeushi

1.    Utamaduni
Mohammed Said Abdulla anadhihirisha utamaduni wa aina mbili.
Kuna utamaduni asilia wa Afrika unaoendelezwa na Aziza na bazazi wa madafu. Aziza anaelezwa kama mwenyeji wa shamba. Aidha anatetea na kudumisha mila za kiafrika kama vile bidii kazini. Anashikilia kuyaishi maisha ya shamba kama vile kutovaa viatu.
Anapuuzilia mbali matumizi ya dawa mswaki na dawa ya meno. Anakataa kuathiriwa na utamaduni wa kisasa.
Utamaduni wa kisasa unaendelezwa nawahusika kama msimulizi, Seluwa, Fedhele na Salma.
Fedhele, Salma na Seluwa wanajipodoa kwa vipodozi na rangi za kisasa.
Msimulizi anatetea uvaaji wa viatu, matumizi ya mswaki wa kisasa na dawa ya kisasa ya meno.
Aidha, msimulizi ni mwanausasa aliyeipata elimu ya kisasa, anaishi kwenye nyumba ya kisasa, anatumia mavazi ya kisasa na vipodozi vya kisasa kama vile kitana.
Selume na msimulizi wanaamkuana kwa kuingiana maungoni; mtindo ambao ni wa kisasa.
2.    Elimu
Elimu ni mfumo wa mafunzo yanayopatikana shuleni, vyuoni au  maishani.
Maudhui ya elimu yameendelezwa kuwili kwenye hadithi ya Mke Wangu.
Kwanza ni yale mafunzo yapatikanayo katika maisha.
Aidha, ipo elimu nyingine inayopatikana vyuoni.
Japo Aziza ni msichana wa shamba, anadhihirisha ukomavu wa hekima. Hii ni ishara tosha kuwa amebobea katikaa mafunzo ya maisha kuhusu maswala ya kazi, ndoa, mahitaji ya jamii na matarajio ya jamii kuhusu wajibu wa mume na mke ndoani.
Msimulizi na Fedhele ni wahusika waliopokea mafunzo ya vyuoni. Wanatajwa kama wahusika waliopokea elimu ya hadi viwango vya juu.
Hata hivyo, elimu hii iliyopokewa na msimulizi inadhihirika kuwa duni kwa sababu haijamwezesha msimulizi kujitegemea. Ni elimu yenye lengo la kupata kazi na wala hailengi kumsaidia mtu kujimudu katika mazingira yake.
Aidha elimu hii inashindwa kumuhami msimulizi na mbinu mwafaka za kuyakabili matatizo ya ndoa. Anashindwa kuidhibiti ndoa yake na Aziza.
Kwa hivyo basi tunaweza kudadavua kuwa mwandishi anaipendelea elimu ya jadi inayompa mtu mafunzo ya maisha dhidi ya ile elimu ya kisasa inayopatikana shuleni na vyuoni.



3.    Utabaka na Utengano
Utabaka ni mfumo wa kijamii unaowagawa watu kwenye makundi kutegemea uwezo wao wa kiuchumi au kijamii.
Kwa upande wake, utengano ni hali ya watu kuwa mbali na wengine. Umbali hiu waweza kuwa wa kiuchumi, kijamii, kijinsia, kimsimamo, kifikra au kimawazo.
Kwenye hadithi ya Mke Wangu, utabaka unajitokeza pale tunapodhihirishiwa utajiri wa wavyele wa msimulizi na wakati uo huo tunadhihirishiwa ufukara wa wahusika wengine kama bazazi wa madafu. Maisha ya bazazi wa madafu nay a msimulizi yanatupa taswra kamili ya utabaka wa kijamii.
Utengano wa kifikra pia unajitokeza kati ya msimulizi na mkewe. Wawili hawa wanaakilisha misimamo pinzani kati ya fikra za jadi na zile za kisasa.



4.    Ndoa
Ndoa ni makubaliano rasmi kati ya mume na mke ya kuishi pamoja.
Ndoa zinazotajwa hadithini ni zile za wazazi.
Ndoa zilizotajwa hadithini ni mbili. Kwanza, ipo ndoa kati ya msimulizi na Aziza. Ya pili ni ndoa kati ya wazazi wa msimulizi.
Ndoa kati ya msimulizi na Aziza inakumbwa na matatizo si haba. Matatizo haya yanachimbuka kutokana na ubaidi wa malezi ya wachumba hawa. Huku msimulizi umuhimu wa vyombo na mienendo ya kisasa, Aziza anasisitiza kuwa mila, desturi na vyombo vya jadi ni lazima vitekelezwe. Ndoa hii inaishia kwa Aziza kumwomba mumewe talaka.
Mwishoni mwa hadithi tunaashiriwa ndoa mpya kati ya aziza na bazazi wa madafu.
Hatuelezwi sana kuhusu ndoa kati ya wazazi wa msimulizi. Hata hivyo ndoa hii inaweza kuelezwa kama ndoa inayoongozwa na kaida za jadi. Hii ni kwa sababu wanamuongoza msimulizi kumuoa mke anayefwata kaida za jadi.


5.      Taasubi ya kiume na matatizo yanayowakumba wanawake
Taasubi ya kiume ni mfumo wa kijamii ambamo mwanamume hupewa nafasi ya juu kumliko mwanamume. Kwenye mfumo kama huu, mwanamume hukumbwa na matatizo si haba.
Jamii ya mke wangu inaweza kuelezwa kama inayoongozwa na mfumo huu.
Msimulizi anabainisha taasubi ya kiume pale ambapo anawalaumu wanawake kwa matatizo yote yanayokumba ndoa. Anapomwona Fedhele na wanaume, anamlaumu fedhele pekee yake na kuwapuuzilia mbali wale wanaume.
Isitoshe, msimulizi anawadharau wanawake na kuwalinganisha na watoto.
Aidha, msimulizi anamlinganisha mkewe na tunda linalostahili kuvimbikwa ili live.
Hata hivyo, japo Aziza ni mwanamke wa shamba, anajitokeza kama mwanamke aliyejikomboa kimawazo na mwenye hekima tele.


6.      Ukengeushi
Ukengeushi ni hali ya mtu kwenda kando na uhalisia wa kijamii. Msimulizi, Fedhele Salma na Seluwa ni baadhi ya wahusika ambao wamekengeuka. Maisha yao hayaingiliani na uhalisia wa mazingira yao.
Japo, fedhele na salma wanajipaka marangi kwa azma ya kuonyesha kuwa wamezinduka, tabia hii inawaudhi wanajamii akiwemo msimulizi. Aidha, tabia ya Fedhele ya kutembea usiku na wanaume inamuharibia sifa mbele ya msimulizi.
Msimulizi naye ni mhusika mwingine aliyekengeuka, licha ya kuwa yeye ni msomi aliyefikia kileleta. Anapigwa chenga na hekima ya msichana wa shamba. Aziza anamdhihirishia kuwa elimu yake haikumfaa kwa lolote bali imechangia kumfumba macho ili asiung’amue uhalisia wa kijamii.
Maswali
Eleza namna maudhui yafwatayo yalivyoendelezwa kwenye hadithi ya Mke Wangu;
i)                    Ndoa
ii)                  Utabaka
iii)                Elimu
iv)                Ukengeushi
5.  MATUMIZI YA LUGHA
Zifwatazo ni baadhi ya mbinu za kisanaa na mbinu za lugha zilizotumiwa kwenye hadithi.
MBINU ZA KISANAA ni mbinu zote zinabuniwa na kutumiwa na msanii kuupitisha ujumbe wake. Hizi ni pamoja na usimulizi, taswira, virejeshi nyuma, maswali balagha, sadfa, chuku, kinaya, hadithi ndani ya hadithi.
MBINU ZA LUGHA pia huitwa tamathali za usemi. Ni matumizi ya vipengele vya lugha vya kimapokeo kama vile methali, nahau, vitendawili, tanakali za sauti, istiari na tashbihi.
1.      Usimulizi uliotumiwa kwenye hadithi ni wa nafsi ya kwanza.
Msimulizi ni mmoja wa wahusika.
Anatusimulia alivyozaliwa na wakwasi, akasoma hadi viwango vya juu na akachaguliwa mke wa shamba na wazazi wake.
Anaendelea kutusimulia kadhia zinazoikumba aila yake na migogoro inayoibuka kati yake na mkewe.
2.      Taswira mbalimbali zinajitokeza kwenye hadithi ya Mke Wangu. Taswira ni picha zinazochoreka mawazoni tunapozisoma kazi za fasihi. Pia huitwa jazanda.
Kutokana na maelezo ya msimulizi, tunapata picha kamili ya Salma, Fedhele na Seluwa. Fedhele na Salma wanachoreka mawazoni mwetu kama wasichana waliojirema na kujipodoa kwa mapambo ya kisasa. Katika ukurasa wa 18, Fedhele anaelezwa kama msichana aliiyevalia kanzu fupi na Salma kama mwenye kujipaka marangi.
Mbali na kuwa mwenye kidomo, Seluwa anachorwa kama msichana mwenye kujipodoa, msichana mcheshi na mwingi wa usasa.
Swali:
Eleza picha inayokujia mawazoni;
Kumhusu msimulizi, Aziza na bazazi wa madafu.
Kuhusu mikono ya msimulizi na nyayo za Aziza.
3.      Hadithi inaanza kwa kirejeshi nyuma. Tunarejeshwa hadi enzi ambazo msimulizi alichaguliwa mke na ninaye. Kirejeshi nyuma hiki ni muhimu katika kuielewa hadithi hii maana kinatupa usuli wa hadithi. Kirejeshi nyuma hiki kinatufafanulia maswala ambayo ni msingi wa migogoro inayoibuka hadithini. Matatizo yanayoikumba familia ya msimulizi yanatokana na vigezo vibovu vilivyotumiwa katika kumchagulia msimulizi mke.
4.      Maswali balagha:
… si lazima kwa hivyo, Aziza awe mwepesi, msikivu, mwelekevu? (uk 18) msimulizi anatumia swali hili kueleza kuwa maadam Aziza kakulia shamba, ni lazima hana jambo. Kwenye ukurasa wa 19, Aziza anatumia maswali balagha kumbeza msimulizi, anauliza;
Mimi nilikuwa nikitazamia nitaolewa na nani katika dunia hii? ...nitapata mume au gumegune tu kama wewe? ...basi wewe ndiye mume wa kunioa miye, we? …huoni wewe wala hupimi?
Katika mazungumzo yake na msimulizi, Aziza anadhihirisha utumizi wa maswali balagha, taja na ufafanue umuhimu wa maswali balagha katika maongezi ya msimulizi. (katika kulijibu swali hili, mwanafunzi atafute na kutaja mifano zaidi ya maswali balagha kwenye hadithi)
5.      Sadfa ni mbinu ya kisanaa ambapo mambo mawili yanatokea kwa pamoja bila kupangwa. Inasadifu kuwa siku ambayo Seluwa alimgeni msimulizi na kumwamkua kwa kumwingia maungoni, bazazi wa madafu anapita akinadi madafu, hapo hapo Aziz anamwita ukumbini, anaomba talaka kutoka kwa msimulizi na kumtaja bazazi wa madafu kama mume wake.

6.      Chuku: ni mbinu ya kisanii inayoeleza jambo kwa namna iliyotiwa chumvi. Katika kuisifia nyayo za miguu yake, Aziza anadai kuwa miguu yake haidungiki kwa miiba. Kwamba hata ukiushindilia mwiba kwenye nyayo zake, mwiba utavunjika!
7.      Kinaya: ni kinaya kuwa msimulizi anayepanga kumchanua Aziza anachanuliwa na Aziza.
8.      Hadithi ndani ya hadithi: kwenye hadithi ya Mke Wangu, msimulizi anaiwazia hadithi ya Nunez ambaye alikuwa chongo na akafikiria kuwa angekuwa mfalme wa vipofu. Hadithi hii inatusaidia kuelewa ung’amuzi wa msimulizi kuwa utamaduni wake na ule wa aziza haungeingiana.
9.      Methali

10.  Nahau na misemo iliyotumiwa hadithini ni pamoja na;
Elekeza rohoni (uk. 18) inayomaanisha kumpenda mtu.
Weka kando inayomaanisha kupuuza
Mtoto mbichi ni msemo wenye maana ya motto mchanga
Tia mguu mjini: pata kufika mjini
Kumvinya mwari: kumwelekeza mtu kwa njia unayotaka wewe
Madarasa: mafunzo
Toa macho: kodoa macho
Zawadi za vicheko: kuchekeshwa
Kumtoa kinyanyaa: kumzindua mtu na kumtoa ushamba

11.  Tanakali za sauti: aliondoka nyatunyatu
12.  Istiara/ istiari
13.  Tashbihi: … kama mtoto anavyonyonya:
…wanawake ni kama watoto wadogo: hii ni kauli ya msimulizi inayotubainishia mtazamo wa msimulizi kuwahusu wanawake.
…ngozi imekacha utafikiri msasa: msimulizi anatumia tashbihi hii kuueleza mkono wa Aziza.