Pages

Mwongozo wa Damu Nyeusi Part 2



SAMAKI WA NCHI ZA JOTO


     Hadithi hii anaanzi wakati ambapo wahusika Zac na Christine wamo chumbani mwa Zac  wakipga gumzo. Chumba hicho kilikuwa na picha ya bob marley ilityorarukararuka  juu ya dawati la zac
Pindi tu Peter ambaye ni rafikiye Zac aliingia. Peter alikuwa muuza samaki wan chi za Joto nje ya nchi hii. Christine alitabasamu kwa geresha alipomona Peter aliyeonekena kuvutiwa na chumba uchwara cha Zac. Zac aliyependa sana kuongea kama Mmarekani,alimkaribisha Peter kitini lakini alikataa kukikalia alikalia kitanda ambapo Christine alikuwa ameketi, Christne alijivuta mbali naye.
   Zac alimwelezea Peter kuwa Christine ni rafiki ya na akawaletea vinywaji. Wakati huo alivunja kimya kilichokuwa chumbani humo na kumwongelesha Christine. Alimuuliza kosi aliyokuwa anasomea naye akajibu akiwa ametabasamu. Baada ya muda mfupi Zac alirudi nyumbani na Christine akamaliza kinywaji chake na kuwaaga alipokuwa njiani alikashifu nafsi yake mbona hakusema jambo lolote la maana.
 Mwishoni mwa juma Zac alimwambia Christine kwamba Peter angetaka amtembelee tena kwani alipendezwa naye na pia anaweza enda na rafikiye Miriam Peter aliishi huko Tank hill.
  Siku ilipowaadia Peter aliwaandalia vinywaji huku wakipga gumzo walitazama video ya ‘Karate kid’. Pindi tu video iliisha Miriam aliongozwa katika chumba cha wageni naye Christine akapelekwa chumbani mwa Peter na Zac akabaki kochini.
  Naye Christine akawa na mazoea ya kwenda Tank Hill. Dadake Christine Dorothy alimwonya Christine kuhusu uhusiano wake na Peter lakini aliipuuza mawaidha ya dadake.
 Christine alitaka kujua jina la pili la Peter lakini alikataa kumwambia kwani alitaka kuheshimiwa  huko Afrika, Baadaye alitambua kwamba  jina lake ni Smithson na alitoka tabaka la chini la wazungu.
Siku moja Peter alimpigia simu Christine aende kwake na alipowasili walianza burudani na baadaye alijipata kitandani mwa Peter . Baada ya miezi Christine aligundua kwamba ni mja mzito  na alijua kwamba kama angemwambia Peter hangefanya lolote na kasha akaamua kuavya mimba. Christine alienda kumweleza Peter,lakini wote hawakutaka mtoto. Christine alitabiri gari iliyokuwa na muziki wenye mapigo ya juu na kuelekea nyumbani.

WAHUSIKA
·         Christine/ msimulizi
·         Zac
·         Peter
·         Deogracias na Wafanyakazi wa Peter
·         Miriam
·         Dorothy
·         Margaret
·         Jagjit na Sunjah Patel

CHRISTINE
Ni msimulizi wa hadithi ya Samaki wa Nchi za Joto. Ni msichana wa wa umri wa miaka ishirini anayesomea Sosholojia katika chuo Kikuu cha Makerere.
Anadhihirika kama mwenye sif zifwatazo;
Kwanza ni msichana msomi kwa sababu tunaelezwa kuwa alisoma hadi Chuo Kikuu. Zac anamueleza Peter kuwa Christine ndiye msichana mrembo zaidi pale chuoni.
Christine anajitokeza kama mdadisi wa mambo, anamchuja Peter na kumuumbua kimaumbile. Anadadisi na kuelewa kuwa Peter alipata faida kubwa kutokana na biashara ya samaki. Samaki ambao anadai kuwa wanarejeshwa na kuuzwa katika maduka ya nyama pendwa. Anang’amua kuwa Peter na Zac walifanya biashara ya bangi.
Kila mara, anaichuja nafsi yake na kujiuliza maswali, anajishutumu kwa kutomwambia Peter jambo la maana. Anayachuja maneno na matendo ya watu kwa makini. Anajihakiki na kuyahakiki matendo yake. Anaigundua japo anaikwepa hali yake ya umaaskini, kudhulumiwa na kudharauliwa na Peter.
Ni mwepesi wa kushawishika. Kutokana na udhaifu huu, Christine anajiingiza katika uhusiano na Peter. Anashawishika kwa haraka kuandamana na Zac hadi kwa Peter. Anashawishiwa na Margaret kuavya mimba. Kutokana na udhaifu huu, anatumiwa na kutupwa.
Unuhimu wa Christine
Ni kielelezo cha wasichana wenye elimu na wajihi lakini wanaoponzwa na ulimwengu kutokana na umaskini na tama.
Isitoshe, Christine anawakilisha dhulma inayofanyiwa wanawake na waafrika kwa ujumla.
Ni kana kwamba mwaandishi anamtumia Christine kutuonya dhidi ya kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi kiholela bila ya kizisikiliza nathari zetu. Matendo na hatma ya Christine inadhihirisha ukweli wa methali, ‘Enga kabla ya kulenga’ / ‘Tahadhari kabla ya hatari’ / ‘Usipoziba ufa utajenga ukuta’ na nyingine nyingi zenye maana sawa na hiyo
Hatimaye, baada yake kutumiwa na kutupwa na Peter, Christine anaamua kurjea kwao pengine akiongozwa na imani kuwa, ‘Mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani’
Maisha ya Christine yanatudhihirishia namna wazungu wanapozitumia raslimali za Afrika na kuzizorotesha kabla ya kuzitupilia mbali.



ZAC
Ni mwanachuo mwenza wa Christine, hivi tunaweza sema kuwa yeye ni msomi. Aidha, Peter ni mwenye bidii kwa sababu tunaelezwa kuwa wakati wa likizo, yeye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Peter.
Anaelezwa na Christine kama kijana aliye na uhalisia, kwamba tofauti na vijana wengine, Zac hakuwa na ndoto za kiuwendawazimu za kuwa watu wakubwa maishani.
Zac anajitokeza kama mwaafrika aliyekengeuka. Anajidhihirisha kama mwafrika anayeiga kuzungumza kwa wamarekani.
Zac ni mshawishi na ndiyo sababu anatumiwa na Peter ili kumshawishi Christine akubali kwenda Tank Hill. Katika ushawishi huu, anajitokeza kama mpenda anasa, anamwambia Christine; … utafurahia matembezi hayo sana, patakuwa na vinywaji vyakula tele na video… (uk 30)
Pia, Zac anajitokeza kama kijana mlevi kwa sababu anapokuwa nyumbani mwa Peter, analewa na kuanza kubwabwaja.
Shughuli zake na Peter zinamdhihirisha kama kijana msiri kwa sababu anajihusisha na shughuli za kuuza bangi bila kutuhumiwa na yeyote.
Umuhimu wa Zac
Zac ni kielelezo cha cha waafrika vibaraka wanaoiga mienendo ya kimagharibi bila kuichuja. Pia, anawaakilisha wafrika wachache wanaotumiwa na wageni kulichafua bara la Afrika kupitia kwa dawa za kulevya na usherati. Zac ni wakala wa peter anayetumiwa kuyapenyeza maovu barani.
Kupitia kwa mhusika Zac, maudhui ya ukoloni mamboleo, ukengeushi, umaskini, usaliti na matumizi ya dawa za kulevya yanaelezeaka.
PETER
Huyu ni mwanamume wa kizungu mwenye umri wa yapata miaka thelathini na tano. Yeye ni mlanguzi wa dawa za kulevya japo anajificha katika biashara ya ununuzi na uuzaji wa samaki. Hivyo anaweza kuelezwa kama mnafiki. Unafiki wake pia unajitokeza pale anapozungumza na Christine kwa upole wakiwa katika chumba cha Zac, (uk 29) upole huu unatoweka pindi tu anapotua mguu afisini pake.
Aidha, Peter ana madharau kwa waafrika. Anawadharau kwa kutoiandika busara inayodaiwa kuibwa kutoka Misri. Anadharau desturi za waafrika na kumbusu Christine shavuni tena kadamnasi ya watu. Pia, anawapa wafanyakazi wake kazi ngumu na kuwaamuru kama nyapara.
Umuhimu wa Peter
Peter ametumiwa kuendeleza maudhui ya ukoloni mamboleo yeye ni mzungu anayeendeleza uozo katika jamii ya kiafrika; Anapunja raslimali ya Afrika kama vile samaki. Anachangia matumizi ya dawa za kulevya, anawaingiza vijana katika ulevi na anasa huku akiwafanya wasahau masomo yao, anawatumia wasichana waafrika kimapenzi na kuwatupa pindi anapomaliza kukidhi haja yake. Isitoshe anahujumu uchumi wa nchi kwa kushiriki biashara ya magendo ya kuuza na kununua sarafu.
Kwa ujumla, matendo ya Peter yanazorotesha uchumi na maadili ya Afrika.
Shughuli zake ni kioo cha kutuonyesha chanzo cha umaskini, upotovu wa kimaadili na unyonge wa watu wa Afrika.
Kupitia kwa mhusika Peter, tunang’amua ukweli wa methali kuwa, ‘vyote ving’aavyo si dhahabu’
DEOGRACIAS NA WAFANYAKAZI WENGINE WA PETER
Deogracias ni mfanyakazi wa Peter wa nyumbani. Mbali naye, pana wafanyakazi wengine afisini pa Peter.
Kwa jumla, wafanyakazi wa Peter ni watiifu, wanamhudumia bwana wao vyema. Aidha, wafanyakazi wa Peter ni waoga. Deogacias anauvumilia uovu utendwao na Peter kwa wasichana wa kiafrika badala ya kuulani. Wafanyakazi wengine wanajitia kufanya kazi Peter anapowatazama.
Umuhimu wa wafanyakazi wa Peter
Wafanyakazi hawa wanaashiria unyonge wa mwaafrika. Unyonge huu umetokana na kubebeshwa mzigo mzito wa kuwatumikia mabwana wa kizungu. Inahuzunisha kuwa wafanyakazi hawa hawafanyi juhudi zozote za kujikomboa.
MIRIAM
Na rafikiye Christine, anaelezeka kama msichana mrembo. Anaelezwa na Christine kama msichana mrefu na mwembamba, mwenye macho ya vikombe Aidha, Miriam ana ujasiri wa kuvuta sigara na kulewa kadamnasi ya watu. Kwa mintarafu hii basi tunaweza kuhitimisha kuwa Miriam amepotoka kimaadili. Utovu wake wa nidhamu unaendelea kudhihirika wakati ambapo yeye pamoja na Margaret wanaunga mkono azma ya Christine ya kuavya mimba
Ulevi wa Miriam unadhihiriika waziwazi wanapomgeni Peter. Analewa na kuanza kucheka sebuleni kivoloya.
Umuhimu wa Miriam
Miriam anawakilisha wasomi waliopotoka kimaadili kwa kujihusisha na uhuni kama vile uvutaji sigara, ulevi na uavyaji mimba.
DOROTHY
Huyu ni dadake Christine mkubwa. Anaelezwa kama mlokole, …Dorothy alikuwa mkristu aliyeokoka…(uk. 31)
Licha ya kuwa mkubwa wa Christine, anakosa ujasiri wa kumkanya mnunawe dhidii ya kuhusiana na Peter. Badala yake, Dorothy anadai kuwa aliota Christine akipewa sumu na wazungu.
Umuhimu wa Dorothy
Kupitia kwa Dorothy, tunapata kufahamu madhara ya kutolikabili tatizo kwa ujasiri. Dorothy ni kielelezo cha jamaa walioshindwa kutekeleza wajibu wa kuwashauri wadogo zao.
MARGARET
Ni dadake Miriam anayefanya kazi ya uuguzi katika zahanati moja jiijini. Utovu wake wa maadili unajitokeza pale anamuunga mkono Christine kuavya mimba. Anaitumia taaluma yake vibaya kuwasaidia wasichana kuavya mimba.
Umuhimu wa Margaret
Anawakilisha wataalamu waliopotoka kimaadili na wanaoongozwa na tama huku wakishirikiana kufanya maovu kama vile uavyaji mimba
JAGJIT NA SUNJAH PATEL
Hawa ni wahindi waliofanya biashara ya magendo na Peter. Mbali na kuwa wajanja wa kufanya biashara ya magendo, wawili hawa nii watu laghai kwa kuwa wanapania kumuuzia Peter noti bandia
Umuhimu wa Jagjit na Sunjah
Hawa wametumiwa kama wahusika wajenzi kwa sababu wanaijenga tabia ya kiulaghai ya Peter. Pamoja na Peter, wanaendeleza hujma dhidi ya uchumi wa nchi.
MASWALI
‘Msimulizi hampendi Peter kwa dhati’, jadili ukirejelea hadithi fupi ya Samaki wa Nchi za Joto.
Jadili uhusika wa Miriam, Dorothy na Margaret katika ujenzi wa wahusika wakuu kwenye hadithi.
DHAMIRA
Yamkini hadithi imelenga kujadili uovu unaoingizwa katika nchi za bara la Afrika na wazungu. Uovu huu ni pamoja na ulevi, ukahaba, ulanguzi wa dawa za kulevya, biashara ya magendo na ukahaba. Azma hii mbi inachangiwa na uwepo wa waafrika wasaliti kama Zac, waoga kama wafanyakazi wa Peter, wasio na msimamo thabiti kama Christine na wale wasio na ukakamavu kama Dorothy.
Margaret na mtaalamu wa unusukaputi ni baadhi ya wataalamu ambao wanatumia maarifa yao na taluma zao kuangamiza jamii badala ya kuiimarisha.
Msimamo wa mwandishi; Japo mwandishi anaelekea kuyahusisha matatizo ya Afrika na wageni, anasisitiza mchango wa waafrika wenyewe katika kujizorotesha.


MASWALI
Je,ni nini suala kuu katika hadithi?
MAUDHUI
Mafunzo yafwatayo yanajitokeza katika hadithi fupi ya Samaki wa Nchi za Joto
Ukoloni mamboleo; Peter anawafanyisha kazi wafanyakazi wake naa kuwatolea amri kama nyapara. Aidha, anawanyanyasa wasichana wa kiafrika kimapenzi.
Aidha biashara ya Peter ya samaki ni ya kujinufaisha yeye binafsi huku akiwapunja waafrika.
Pia, anawatumia vijana kama Zac kwa manufaa yake ya kibinafsi
Usaliti; Zac anausaliti urafiki wake na Christine kwa kumuongoza kuingia katika urafiki na Peter. Licha ya kujua tabia za Peter, Zac anamshawishi Christine kuingia katika urafiki naye.
Vilevile, Christine anazisaliti hisia zake. Ni bayana kuwa hisia za Chrisine zinamuonya dhidi ya kujiingiza katika urafiki na Peter. Hata hivyo anazipuuza na kujitia katika urafiki uliomsababishia madhara tele.
Mapenzi; mapenzi yanayojitokeza katika hadithi yametawaliwa na unafiki na usaliti.
Zac anajifanya rafiki wa Christine lakini hatimaye anamsaliti kwa kumtaka ashiriki mapenzi na Peter.
Peter naye ana mapenzi ya uongo kwa Christine. Anajifanya kama mwenye kumjali lakini Christine anaposhika mimba na kuavya anampuuza na kumtupa. Inaelekea kuwa alimpenda tu kwa muda ili kukidhi haja yake ya muda.
Yamkini Christina naye anampenda Peter kutokana na dhifa kedekede alizoandaliwa pamoja na zawadi mbalimbali alizompa.
Ulanguzi na Matumizi ya dawa za kulevya; maudhui haya yanaendelezwa na Peter pamoja na Zac. Tunaelezwa kuwa Zac alimtafutia Peter bangi.
Ukengeushi; huku ni kupotoka na kutenda mmbo kinyume na matarajio ya jamii. Zac ndiye mhusika aliyekengeuka sana.
Anajitia kutaka kuzungumza kama mmarekani mweusi. Pia, hataki kuzungumza Kiganda na Deogracias, badala yake, yeye anazungumza Kiingereza.
Tabia ya Miriam kulewa na kuvuta sigara kadamnasi ya watu haitarajiwi katika jamii ya Afrika.
Aidha, suala la kupigana busu hadharani halikubaliwi na jamii ya afrika. Hivi basi, Christine anakengeushwa na mienendo ya Peter ya kumbusu hadharani.
MASWALI
Eleza namna maudhui
Utabaka, Elimu, Ubarakala na ulaghai, Matatizo ya wanawake


DAMU NYEUSI

      Ni hadithi inayomhusu  Fikirini ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya Uzamifu aliyeenda kusomea Marekani. Huko uzunguni anakutana na changamoto za kubaguliwa kwa rangi ya na wazungu na weusi wenzake.
    Hadithi iaanzapo anaachwa na basi ambalo linaendeshwa  na mzungu kwa kushukiwa kuwa jambazi. Hatimaye anakumbuka  alivyofikishwa mahakamani na kupigwa faini baada ya kuitwa plisi na mwanamke mzungu aliposahau  kufunga zipu ya suruali yak. Aliona kwamba kama angekuwa Afrika,ndugu zake wangemfanyia hisani badala ya kumwitaia polisi. Jaji mweusi  alimtoza faini ya dola mia mbili na kuepuka kifungo cha miezi sita gerezani.
  Baadaye alipokuwa akitembea kuelekea  shuleni,alipatana  na mwanamke mweusi ambaye alimwalika nyumbani mwake. Fikirini hakujua nia yake lakini mwanamke huyo alikuwa amemweleza kuwa atampeleka hadi chuoni lakini kwanza waingie nyumbani mwake.Wakiwa humo ndani, ndugu yake mwanamke huyo aliufunga mlango.Fiona alianza kumwitisha pesa alizo nazo lakini hakuwa nazo. Alijaribu kutoroka alipohisi kwamba yumo hatarini lakini Fiona alimwita Bob na kumweleza kwamba Fikirini alikuwa anajaribu kumbaka. Bob alimwambia Fikirini auwachilie mkoba wake naye Fiona kamwambia avue nguo zote. Baada ya kuchakurachakura mifuko yake na kupata hamna kitu, Bob alimwachilia na kumwambia asirudi huko tena. Fiona alikataa aachiliwe na kudai kuwa angetaka kumuua. Hatimaye, Fikirini aliachiliwa huru akiwa tupu na akakimbia kama mtu aliyepagawa.
  Ijapokuwa Fikirini aliviacha vitu vyake nyuma,kama vitambulisho,alimshukuru  Mungu kwa kumwachia uhai wake.
DHAMIRA
Mwandishi anazungumzia kuhusu ubaguzi kati ya wazungu na weusi na pia weusi na weusi. Dhamira ni kuwa mwandishi anakashifu swala la ubaguzi wa rangi.
MAUDHUI
1.UBAGUZI WA RANGI.
    Watu wenye rangi nyeusi wanabaguliwa na wazungu au weusi wenzao.Anabaguliwa barabarani kuwa yeye ni jambazi.
Pia chuoni anabaguliwa.Anapewa alama chache ingawa anafanya vizuri katika mtihani. Weusi wenzaka wanabagua kwa vile ametoka Afrika na ameenda kuwaharibia.
2.ELIMU.
Fikirini alienda huko kutafuta elimu ambapo alikuwa anasomea shahada ya uzamiifu.
3.UJAMBAZI
  Fikirini alikutana na majambazi wawili aliowaita ndugu  zake lakini walimvamia na kumtupa nje akiwa tupu.
4.UVUMILIVU.
  Fikirini aliweza kuvumilia matatizo mengi kama ubaguzi ili awezekumaliza masomo yake na kurejea nyumbani.
5.USALITI.
  Dadake” Fikirini aliisaliti imani yake kwa kumhadaa.
6.UKATILI.
“Dadake” Fikirini alikuwa anataka kummaliza Fikirini kwa sababu ya kukosa pesa.
7.UNAFIKI.
  Huyo “dadake” alijifanya mwema ili amsaidie Fikirini lakini alikuwa na nia yake.
WAHUSIKA.
1.FIKIRINI.
Ni mwanafunzi na ametoka katika nchi za Afrika.
SIFA
Ø Ni  mvumilivu,amevumilia ubaguzi;baridi na dhuluma
Ø Ni msomi,alienda uingereza ili aweze kumalizia masomo yake ya shahada
Ø Ni mwoga,alijisaidia aliposhikwa na woga
Ø Mwenye imani,aliamini kwamba Fiona angeweza kumsaidia kwa gari lake nzee ili ampeleke chuoni.
Ø Mpole,alipoulizwa maswali ya upuzi wenzake alivumilia
Ø  Mwenye bahati mbaya (mdubira),alisahau kufunga  zipu ,alipatana na majambazi.
Ø Mjinga,aliamini kwa haraka kwamba “dadake” angemsaidia.
Ø Mzalendo,aliipenda nchi yake.

2.WAZUNGU.
SIFA
Ø Ni wenye ubaguzi mwingi .
Ø Ni wenye imani potovu,wanaamini kwamba Waafrika ni kama nyani.
3.FIONA NA BOB.
Ni wamarekani weusi.
Ø  SIFA
Ø Ni majambazi.
Ø Ni wakatili,badala ya kumsaidia mtu akiwa na shida  wanazidisha
Ø Fiona ni mnafiki,alijifanya kumsaidia Fikirini ila ana zake.
MTINDO
1.USIMULIZI
Masimulizi ya mwandishi yanatumia nafsi ya tatu
2.KUCHANGANYA NDIMI.
Fikirini aliulizwa“Do youspeak English?”“ someone called to say you are exposing yourself.”
“How you doing?”                                                                                                                                                                                                                                     “Am cool”                                                                                                                                                                                                         “I say remove your clothes or else”                                                                                                                                                                                “ I say shoot him Bob”


MATUMIZI YA LUGHA.
1.METHALI.
Ø Nyumbani  ni  nyumbani  ingawa  ni pangoni - Ilitumiwa na Fikrini alipokuwa akirejelea kwao nyumbani ambako ni Afrika naye ako uingereza ambako ni kuzurui kuliko kwao lakini hata kama kwao si kuzuri ivo ni nyumbani.
Ø Baharia wa pemba hufa maji mazoea - mabaharia wa Pemba wamezoea kufa mali na ni jambo la kawaida.
Ø Simba akikosa nyama hukula nyasi – Fikirini alikosa chakula kizuri cha kukula kwa hivyo alilizimishwa kula chakula chao.
Ø Siku ya kufa nyani miti yote huteleza – Siku ya mkosi ni  mkosi na hakuna jinsi ambavyo mtu anaweza kuepuka.
2. TANAKALI ZA SAUTI
Pepesuka pepesu pepesu.
Ø Nyapia nyapu nyapu
Ø Nyeupe pepepe
3.MISEMO

Ø Mlevi chakari – mtu aliyelewa kupindukia .
Ø Maji yamezidi unga – mambo kuzidi matarajio
Ø Kusalimu amri – kukubali.
Ø Kufa ganzi – kupoteza fahamu
Ø Elewa fika.

2 comments: